Sunday, December 21, 2008

Shida Za Watanzania Zitaisha lini?


Watanzania Wanahitaji kudai Uhuru Wao.
Nadhani Tanzania iko chini ya Advanced Neocolonialsim ambapo uchumi umeshikwa na watu wa nje, wakati serikali imeshikwa na watanzania wasiokuwa na mapenzi na nchi hii na tayari ama wana maskani yao nje ya nchi au wana mipango ya namna hiyo.Kwa nini?(a) Aliyekuwa Gavana wa Benki kuu akisimamia wizi mkubwa wa pesa zetu, baada ya kuacha ofisi alirudi kwake Marekani, ambako ndiko alikomalizia maisha yake. (b) Aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali akisimamia mikataba mingi mibovu, amegundulika kuwa na vijisenti vingi sana huko kwenye mabenki ya nje. Siku yoyote akitaka ataondoka na kwenda kwenye vijisenti vyake. Huyu bwana naye alikuwa ametushikia bendera ya karatasi tu. (c) Aliyekuwa katibu Mkuu wa wizara ya fedha akisimamia matumizi na mapato ya serikali yetu ana maskani yake ya kudumu huko Marekani. Siku yoyote anaweza kuondoka.(d) Leo hii nimesoma headline moja kuwa aliyekuwa waziri wa elimu akisimamia kuharibika kwa elimu nchini ili vizazi vijavyo viweze kutawaliwa kirahisi naye ana mpango wa kuhamie Marekani.(e) Kuna tetesi kuwa kiongozi mmoja mzito sana anauza mali zake kwa kasi sana, inawezekana lengo lake ni kuhamia nje ya nchi kutokana na mwenendo wa kesi za ufisadi zilizoanza. Kiongozi huyu anasemekana ana majumba Marekani na Afrika ya Kusini.(f) Viongozi wetu wengi waliowahi kushika nafasi nyeti wana maskani mengine nje ya nchi wakati hakuna viongozi wa nchi za nje walio na maskani yao nchini mwetu.Huu ufisadi tunaosikia kila siku ni matokeo ya viongozi wetu kuitumia nchi yetu kama sehemu ya wao kuchuma, halafu wakalie walichochuma huko nchi za nje. kwa kifupi, tunahitaji uhuru wetu tena, safari hii ikiwa ni dhidi ya Advaced Neocolonialism.

No comments: