Monday, May 4, 2009

My Tianjin!

This is the City where I'm spending my 4th year,I love it even if it is somehow polluted!














Sunday, March 15, 2009

Safari yangu ya kwenda Iwindi Kijijini kwangu




Baada ya miaka zaidi ya mitatu kutoonana na mama,babu na wote nyumbani at last nimekutana nao na kuwakuta wazima na wao hawajaamini kuniona mwanao baada ya muda mrefu sana.Haha!I miss u all again ...


















Even people who are not my relatives they all missed seeing me,That is amazing!





My trip to Tanzania...


My Trip to tanzania(home)...Was really nice!













Nimekutana na Majid Mjengwa Dar

My holiday was nice and nilifurahi sana pale siku moja nilipokuwa nikipata kifungua kinywa cha maziwa,chapati na vitumbua katika mgahawa mmoja pembeni mwa Lumumba road.Huyu kaka namkubali wa kuweka picha za kuonesha the really Tanzania kwa kila kona ya nchi,hata kule kusikofikika yeye hufika.
All the best bro in your majukumu!



Saturday, January 10, 2009

AIDS in Mbeya and Iringa??!!

Katika Kijarida cha Habari za Ukimwi (April - June 2008) Takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya Ukimwi kufuatia Kampeni ya Kitaifa ya Kupima Ukimwi kwa Hiari ni kama Ifuatavyo:Maambukizi ya Juu:- Mbeya - 15.2% (Kyela 24%, Chunya 23.7%)- Iringa - 14.7% (Ludewa 19.7%, Makete 16.8%) - Dar Es Salaam - 8.3%- Mwanza - 8.1 %- Coastal - 6.2%- Ruvuma - 5.6%Hakuna sababu zilizoainishwa ni nini vichocheo vikubwa vya maambukizi haya.Wazalendo, Tunaambiwa Elimu Kuhusu Ukimwi imewafikia Watanzania kwa kiwango cha kutosha ikiwa ni pamoja na jinsi ya kujikinga na maabukizi. - Je, ni nini vichocheo vya maambukizi makumbwa yaliyoainishwa hapo juu na ni nini kifanyike?

Wednesday, January 7, 2009

Ziwa Ngozi!

Ziwa Ngozi linalodaiwa kuhamishwa kwa jiwe la moto 2009-01-06 13:50:37 Na Thobias Mwanakatwe
Tanzania ni nchi iliyobahatika kuwa na maziwa mengi hata hivyo kila ziwa lina historia yake jinsi lilivyojitokeza kwa maana ya chanzo chake. Ziwa Ngozi lililoko Rungwe ni moja ya maziwa ambayo wenyeji huogopa kulitembelea kutokana na imani walizonazo. Mwandishi Wetu, Thobias Mwanakatwe, anaandika zaidi. Yapo maziwa au maeneo ambayo ukianza kusimuliwa historia yake unaweza kabisa ukakata tamaa hata kulitembelea hasa kutokana na maajabu yaliyopo katika ziwa hilo. Mojawapo ya maeneo yenye historia ya maajabu ni ziwa Ngozi lililopo katika kijiji cha Mbeye One wilayani Rungwe katika mkoa wa Mbeya. ``Mimi sijawahi kufika huko lakini siwezi kwenda kule kunatisha,`` anasema Uswege Mwakimbete alipoulizwa kama amewahi kufika kwenye ziwa hilo. Ziwa hilo liko urefu wa mita 150 kutoka kilele cha milima inayozunguka ziwa , ambapo kutoka usawa wa maji kina cha maji ni urefu wa mita 73 na ukubwa wa eneo lenye maji ni kilomita sita hadi 10 za mraba na lina ukubwa wa kilometa za mraba 3.75. Wataalam wanaeleza kuwa ziwa hilo limetokana na volkano , limezungukwa na misitu mizuri ya asili ya kitropiki hali nzuri ya hewa na tulivu. Ili kulifikia ziwa hilo unalazimika kutembea kwa mwendo wa kati ya dakika 45 na saa 1 kutoka kijijini Mbeye One ambacho kipo barabara kuu ya Mbeya-Kyela. Pia kutoka katika kilele cha milima inayozunguka ziwa hilo unalazimika kushuka kwa zaidi ya dakika 45 huku ukilazimika kushuka kwa kutumia mizizi migumu ya miti ya asili iliyopo katika msitu mnene kwasababu ya mteremko mkali kuelekea katika ziwa hilo. Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbeye One, Watson Mwakalinga anasema kuwa ziwa hilo liligunduliwa mwaka 1925 ambapo anasema kuwa ziwa hilo lilihama kutoka katika kijiji cha Mwakaleli wilayani humo baada ya kudaiwa kuwa baada ya kuchomwa na jiwe la moto na wakazi wa kijiji hicho. Anasema ziwa hilo la maajabu lilichomwa moto na wakazi wa kijiji cha Mwakaleli kwasababu lilikuwa likileta mikosi mingi kijijini hapo ikiwemo watu kufa kila mara hali iliyowalazimu wazee wa kijiji hicho kufanya uchunguzi na kubaini kuwa kunasababishwa na ziwa hilo la Ngozi. Hata hivyo unapowauliza wataalam wa masuala ya mazingira wanasema kisayansi ziwa haliwezi kuhama. ``Kwa vile ziwa hili halikuwepo pengine wangesema kuwa halikuwepo mpaka volkano hiyo ilipokuwepo lakini ziwa haliwezi kuhama,`` anasema Prof .William Rugumamu , wa Idara ya Jiografia toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwakalinga anasema anasema kuwa maajaabu ambayo yametokana na imani za kishirikina yanayodaiwa kuwepo katika ziwa hilo ni pamoja na watu wanaofika huku kudaiwa kupotea, sauti za vikohozi vya watu wasioonekana pamoja na miujiza ya watu wanaotwanga mahindi lakini hawaonekani. Anasema mbali ya maajabu mengine ya imani za kishirikina yaliyokuwepo, anasema kuwa ziwa hilo linatabia ya kubadilika rangi ambapo anasema ziwa hilo limekuwa likigeuka rangi mara kwa mara na kuwa na rangi za kijani, bluu, nyeusi na nyeupe. Anasema kubadilika kwa maji katika ziwa hilo kimsingi wananchi wameshindwa kufahamu kunatokana na nini ingawa waatalam waliowahi kufika kijijini hapo wanadai kunatokana na mabadiliko ya hali ya hewa ya eneo hilo. Prof. Rugumamu anasema hali ya kubadilika rangi kwenye ziwa Ngozi siyo kitu cha ajabu kwani ni hali inajitokeza kwenye maji ya bahari ambapo anasema wakati mwingine huweza kuonekana rangi ya bluu au rangi ya upinde kutegemeana na hali ya jua. `Kwenye maji ya bahari hali ya maji kubadilika ni jambo la kawaida pengine watu hawawi makini kuangalia tu,`` anasema Prof. Rugumamu ambaye ni mtaalam wa masuala ya mazingira na hali ya udongo. Hata hivyo unapofika eneo hilo misitu inayozunguka ziwa hilo ina hali nzuri pamoja na baadhi ya wanyama wakiwemo chui na nyani, ingawa ni ni nadra sana kuwaona chui katika misitu hiyo kwa kuwa wanajificha na hawajawahi kuleta madhara kwa binadamu. Anasema kutokana na maajabu hayo, wakazi wa kijiji hicho walikuwa wakiogopa kabisa kufika katika ziwa hilo kutokana na maajabu hayo yaliyokuwa yakisemwa. Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Mbeye 1, George Mbepe (65), anasema awali walikuwa wanahofia kufika katika ziwa hilo kutokana na madai ya kuwapo kwa imani za kishirikina. ``Kulikuwa na imani kuwa mtu akija huku atasikia vikohozi vya watu wasioonekana huku wengine wakitwanga mahindi, lakini hawaonekani,`` alisema na kuongeza kuwa imani hizo zilisababisha watu wasifirie kwenda katika ziwa hilo . Hata hivyo anasema, kuwa kutokana na maji hayo kuonekana yanafaa, yamekuwa yakitumiwa kama mradi na vijana ambao wamekuwa wakiuza kati ya shilingi 300 na 500 kwa lita. Wakazi wa Kijiji hicho, wanaamini maji ya ziwa hilo hutumika kama dawa kwa ajili ya kutibu watoto ambao wamekuwa wakistuka nyakati za usiku na kwamba pindi wanaponywesha maji hayo hali hiyo inakoma mara moja. Prof .Rugumamu anasema kuwa hakuna maelezo yoyote ya kisayansi ya Ngozi kuwa na uwezo wa kuponya magonjwa lakini anasema wenyeji kwenye maji mengi yanayotokana na volkano wamekuwa na imani za aina hiyo. ``Hata sehemu nyingi ambako yanatoka maji moto yanayotokana na volkano watu wanaamini hiyo lakini hiyo ni imani tu, anasema .`` Ziwa hilo liliwahi kupandikizwa samaki aina ya perege mwaka 2001, hata hivyo hadi sasa hawajafanikiwa kuvua samaki hata mmoja kutokana na ukosefu wa vifaa vya uvuvi pamoja na ugumu wa kufika katika ziwa hilo . Hata hivyo imani hizo za kishirikina za wakazi wa Kijiji hicho zilifikia tamati mwanzoni mwa mwaka huu baada ya timu ya watafiti wa Kimataifa kutoka nchi za Ufaransa, Uingereza na Ubelgiji kufanikiwa kufika katika ziwa hilo na kufanikiwa kuingia ndani ya ziwa hilo na kuchota udongo kwa ajili ya kufanya utafiti wa kisayansi kuhusiana na ziwa hilo pamoja na mazingira yanayolizunguka. Watafiti hao walibaini kuwa ziwa hilo lina umri wa zaidi ya miaka 40,000.Ingawaje wataalam wengine wanasema kuwa ziwa hilo linaweza kuwa lilikuwepo hata miaka milioni 2 iliyopita. Kuna baadhi ya watalii wamekuwa wakitembelea ziwa hilo ambapo hulipia kiasi cha Sh 2,000 kwenda kuliona . Hata hivyo baadhi ya wananchi wanasema kuwa kiasi kinachotozwa cha sh.2,000 hakitoshi bali wangetozwa zaidi. ``Watalii walitakiwa kutozwa shilingi 10,000 na watanzania walipe shilingi 2,000 ili mapato yatokanayo na shughuli za utalii yaweze kutumika kwa shughuli za maendeleo katika Kijiji na wilaya,`` anasema Jackson Mwakabuta,mkazi wa kijiji hicho. Mwakabuta anasema kuwa idadi ya watalii wanaotembelea vivutio vya utalii wilayani humo haitoshelezi, ambapo alisema kuwa kuna haja ya kufanyika kwa juhudi za makusudi kutangaza vivutio vilivyopo nchini pamoja na kuwahamasisha Watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii badala ya kuwategemea wageni tu. Mbali ya ziwa hilo kukosa watalii wanaotembelea kuangalia vivutio vilivyopo, pia wakazi wa Kijiji cha Mbeye One, wameshindwa kuendesha shughuli za uvuvi kutoka katika ziwa hilo kutokana na ukosefu wa vifaa vya uvuvi pamoja na ugumu wa kufika katika ziwa hilo la shimo ambalo limezungukwa na milima. Wananchi hao wanaiomba serikali iwasaidia kupata boti itakayotumika kwa shughuli za uvuvi katika ziwa hilo, ambapo alisema kuwa kuanza kwa shughuli za uvuvi kutasaidia kukuza uchumi wa kijiji hicho na hivyo kuinua maisha ya wananchi . Mwambata wa Ubalozi wa Ufaransa nchini, Dk. Raymond Latest ambaye alikuwa pamoja na timu ya utafiti wa ziwa hilo anasema kuwa wilaya ya Rungwe ina vivutio vizuri vya utalii kuliko mkoa wa Arusha lakini havifahamiki kutokana kwa kutotangazwa. Anasema awali kabla hajafika nchini, alikuwa akiifahamu zaidi nchi ya Kenya ambayo imekuwa ikijitangaza zaidi kwenye utalii, lakini alipofika nchini akagundua kuwa Tanzania ina vivutio vingi vya utalii ikiwamo misitu ya asili kuliko nchi yoyote ya Afrika Mashariki. Dk.Latest anasema vivutio hivyo vikitangazwa vizuri vitaweza kuchangia kukuza pato la Taifa kupitia sekta ya Utalii. Akilizungumzia ziwa Ngozi, Dk. Latest alisema kuwa amevutiwa na ziwa hilo lililozungukwa na milima na kuonekana lipo shimoni pamoja na kuzungukwa na misitu ya asili, ambapo alisema kuwa atahakikisha anaitangaza wilaya ya Rungwe ili iweze kufikiwa na watalii wengi kutoka nchini Ufaransa na watalii waweze kujionea maajabu ya wilaya hiyo. Kiongozi wa timu ya watafiti, Dk. David Williamson kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anasema hiyo ilikuwa mara yao ya kwanza kufika katika ziwa hilo kwa lengo la kufanya utafiti ili kujua umri wa ziwa hilo, mabadiliko ya hali hewa na mazingira pamoja na kufahamu volkano ndogo ya mwisho ililipuka lini. Na kama maji ya ziwa hilo yanafaa kwa matumizi ya binadamu. Dk. Williamson anasema kuwa ziwa ngozi ni moja kati ya maziwa 10 ya volkano yaliyopo wilayani Rungwe ambayo wanafanyia utafiti wa kisayansi, aliyataja maziwa mengine kuwa ni pamoja na Ndwati, Kisiba, Chungululu, Ikapu, Itamba, Asoko, Ilamba, Kingili, Katubwi na Itende. Utafiti wao unajumuisha uchukuaji wa vumbi na tope lililopo chini ya ziwa hilo vitu ambavyo vitasaidia katika utafiti wao. Katika utafiti wao wa awali waligundua kuwa kina cha maji katika ziwa hilo kinazidi kupungua kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, mmonyoko wa udongo na kwamba hali hiyo inahatarisha uwepo wa ziwa hilo kwa miaka ijayo. Akieleza sababu za kuchukua tope lililochini ya ziwa hilo , alisema kuwa wanaamini kuwa tope lililoganda ndani ya maji linakuwa na mkusanyiko wa tabaka mbalimbali za taka, udongo na kwamba kiasi wanachochukuwa kitawawezesha kujua mambo muhimu wanayoyahitaji katika utafiti wao. Mtafiti mwingine kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ,Edister Abdallah anasema kuwa utafiti huo utasaidia wakazi wanaosihi kuzunguka ziwa hilo kuendana na mabadiliko ya hali ya hewa hivyo kushiriki katika kuhifadhi mazingira ya eneo hilo na wilaya ya Rungwe na hivyo kufanya uwepo wa ziwa hilo kuwa endelevu. Anasema kuwa juhudi za dhati zinapaswa kuchukuliwa ili kuwajengea wananchi utamaduni wa kutunza mazingira tofauti na ilivyo sasa ambapo wananchi hawaoni wajibu wao wa kushiriki katika kutunza na kuhifadhi mazingira ambayo ni muhimu katika maisha ya mwanadamu na viumbe hai. Alisema kuwa wananchi wakipatiwa elimu na kujua umuhimu wa kuhifadhi mazingira kila mmoja atatimiza wajibu wake kwa kutunza mazingira. Anaongeza kuwa ukosefu wa elimu umekuwa ukisababisha wananchi wengi washiriki katika uharibifu wa mazingira bila wao kujua au wengine kuharibu kwa makusudi bila kujua athari za baadaye za uharibifu huo. Naye Mshauri wa Sekta ya Wanyamapori mkoa, Stanley Munisi anasema mkoa wa Mbeya unao vivutio vingi vya kitaalam, lakini vingi bado havijatangazwa na kwamba hivyo ipo mikakati ya kuanza kuzitangaza.

Tuesday, January 6, 2009

Chifu ataka CCM isichaguliwe Mbeya

Chifu ataka CCM isichaguliwe Mbeya
Na Brandy Nelson, Mbeya
CHIFU mkuu wa kabila la Wamalila, lililo katika tarafa ya Isangati wilayani Mbeya Vijijini, Golian Mpoli, 90, amewataka wananchi wake kutokichagua chama
ambacho kinawanyima maendeleo na badala yake wamsubiri mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sambwee Shitambala, katika uchaguzi wa mwaka 2010.
Mgombea huyo alienguliwa kwenye kinyang'anyiro cha kiti cha ubunge cha jimbo la Mbeya Vijijini baada ya kugundulika kwa kasoro kwenye kiapo chake. Vyama vya CCM na CUF vilibaini kasoro hizo na kuweka pingamizi ambalo lilikubaliwa na Tume ya Uchaguzi.
Lakini chifu huyo wa kabila la Wamalila anaona kuwa bado kuna haja ya kumsubiri mgombea huyo katika uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa hawana la kufanya kwa sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Chifu Mpoli, akiwa na mkalimani kutokana na kutojua vizuri lugha ya Kiswahili, alisema kuwa toka uhuru wamekuwa wakitawaliwa na viongozi wa CCM, lakini hakuna maendeleo yoyote ambayo chama hicho kimewapa zaidi ya kuendelea kuwanyonya.
Alipoulizwa kuwa ni kwanini anamtaka Sambwee Shitambala kuwa mbunge wa jimbo la Mbeya Vijijini wakati hajawahi hata kuwaongoza na pia si mzaliwa wa tarafa hiyo ya Isangati, Chifu Mpoli alisema kuwa kutokana na jinsi alivyomuona na kutafakari anaamini anaweza kuwasaidia wananchi wake.
"Tangu afariki mbunge wetu Edward Shiwa aliyetuongoza kipindi cha mwaka 1995 hadi 2000, tulikuwa hatuna shida yoyote kwa kuwa alikuwa anatusikiliza na kutatua shida zetu na alianza harakati za kuleta umeme. Alifikia hatua ya kuwekwa nguzo na bahati mbaya akafariki dunia kabla ya kulimalizia," alisema.
Alisema tangu alipoondoka mbunge huyo bado nguzo hizo zimelazwa chini na
nyingine zimechimbiwa, lakini hakuna maendeleo yoyote ya suala la kupata umeme kwa wananchi wa tarafa hiyo.
Chifu huyo alisema kuwa Mbunge Shiwa ndiye aliwaletea wazo la kujenga Shule ya Sekondari ya Ilembo na kwamba baada ya hapo tangu mwaka juzi wamekuwa wakichangishwa fedha kila mara kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, lakini hakuna kinachoendelea.
"Baada ya kuondoka Mbunge Shiwa, kuna wabunge wa CCM walikuwepo lakini hakuna walilotufanyia kama huyu wa mwisho... pamoja na kuwa mimi ni chifu mkuu nilikuwa simfahamu... nilikuwa nasikia jina tu mpaka alipofariki dunia. Hivyo kwa niaba ya machifu wenzangu na wananchi, hatuitaki CCM... tunamsubiria Sambwee Shitambala mwaka ujao, ndiyo maana nimeamu kuja huku kuwaeleza," alisema.
Alipoulizwa sababu za kutoitaka CCM, chifu huyo alijibu kuwa viongozi wake wanawanyonya wananchi na wamekuwa na matatizo mengi katika eneo hilo lakini viongozi wa CCM wanashindwa kutatua na kwamba tayari kikao cha machifu kimefanyika katika kujadili suala hilo na kwamba wamekubalina wamsubiri Shitambala mwaka 2010 ili aweze kuwasaidia katika kusukuma gurudumu la maendeleo.
Wakiongea na Mwananchi, baadhi ya wananchi wa kata ya Ilembo walisema kuwa kitendo cha kuondolewa mgombea wa Chadema ni sawa na kunyang`anywa tonge la ugali mdomoni kwa kuwa hali hiyo imewasikitisha sana.
Walisema kuwa kati ya wabunge watatu waliowahi kuongoza jimbo la Mbeya Vijijini, ni Shiwa (CCM) ndiye aliyeweza kuwaletea maendeleo hivyo bado anahitaji mabadiliko na kwamba msimamo wao ni kuchagua chama pinzani.
"Kama Mbunge Yete Mwaliyego ambaye alichaguliwa mwaka 2000 huyo ndiyo hatusemi kwani alikuwa anaomba kura kwa mabavu na alifikia hata kutuambia kuwa mnichague msinichague mimi ni mbunge wenu tu na alipochaguliwa hakuonekana tena hadi naye alipofariki dunia," alisema Sipiti Solomoni wa Kijiji cha Ilembo.
Alisema kuwa wao ni wanachama wa CCM na wana kadi za CCM, lakini dhamira yao ilikuwa ni kumchagua mgombea wa Chadema kwa kuwa ndiye alikuwa chaguo lao hivyo kwa sasa hawana la kufanya.
"Kweli suala la mgombea wa Chaema kuondolewa limetuumiza sana tulikuwa tunampenda na bado tunampenda na tunamuhitaji awe mbunge wetu kwani ndiye tuliyemdhania kuwa angeleta mabadiliko katika jimbo hili... labda kama anaweza kupita huyo wa CCM wakimchagua kwani anasema kwa yeye katumwa na Mungu aje kuwa mbunge," alisema.
Walisema kuwa wanahitaji mabadiliko kwani CCM imekuwa ikiwahaidi lakini hakuna mafanikio yoyote na kwamba wamechoka na chama hicho ambcho wamekuwa wasikilza kiula mara sera zake lakini hakuna zinazotekelezwa katika eneo hilo.
"Msimamo wetu ni ule ule wa kutaka mbunge kutoka katika chama cha upinzani. CUF wamekuja hapa tumewasikiliza sera zao na tunawasubiri kuona sera zao ni nini kama tunaona nao hawaturidhishi, basi tutajua la kufanya," alisema mmoja wao.
Wananchi hao ambao walikuta wamesimama katika vikundi vikundi maeneo ya klabu cha pombe na sokoni katika kijiji hicho cha Ilembo ambacho rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi alizindua kampeni za CCM.
Walipohojiwa kama wangeenda kwenye mkutano huo wa uzinduzi, walisema kuwa wangeenda kwa ajili kumfahamu rais huyo mstaafu kwa kuwa hawajawahi kumuona.

Mboma: Kitambi kimeniangusha

mambo ya Home!
Mboma: Kitambi kimeniangusha
Hawa Mathias, Mbeya
ALIYEKUWA Mkuu wa Majeshi Nchini, Meja Jenerali, Robert Mboma, amesema anaamini kitambi alicho nacho kimesababisha kushindwa katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) za ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini.
Mboma aliyasema hayo juzi wakati akiwashukuru wananchi katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho za kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo.
Alisisitiza kuwa anaamini kilichochangia kutopata kura nyingi zaidi ni kitambi
hicho alichokuwa nacho na kwamba hali hiyo itamkomaza kisiasa.
Mboma ambaye aliwashangaza baadhi ya watu walioshuhudia uzinduzi wa kampeni hizo uliofanywa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi katika kijiji cha Ilembo Mbeya vijijini.
alisema kkuanguka kwake katika jimbo hilo kumetokana
na wananchama wa chama hicho kumnyima kura.
Alisema kitendo hicho hakiotamuathiri bali wanamkomaza kisiasa na kwamba endapo kama angeteuliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo angelepeleka maendeleo.
"Kwa kweli nanawashukuru wananchi mlionipigia kura nilizozipata ingawa hazikuwa
ndogo lakini ninasikitika na ninawashukuru ambao hawakunipigia kura na kuniangusha wakati wakijua wazi kuwa mimi ni mzaliwa na hapa na mngenichagua ningewaletea wananchi maendeleo katika jimbo la Mbeya vijijini," alisema.
Aliendelea kusema kuwa sio mbaya hata kama wamemchagua Mchungaji Mwanjali kwa sababu anaimani atawaletea Maendeleo na kurithi yale yote aliyatarajia
kuyafanya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Marehemu Richard Nyaulawa katika
kuboresha huduma za jamii hususan maji, umeme na kuboreshea miundombinu.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya David Mwakyusa aliwatahadhalisha wapiga kura kuwa makini na Vyama vya Siasa hususan Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) a kwa kuzingatia sera zao na kwamba wawafananishe na Vyura wanaosubili kipindi cha Mvua na kuanza kukoroma katika mito.
Alisema vyama vya upinzani vinatakiwa kuangaliwa kwa umakini na kwamba kipindi hiki cha kampeni wanaanza kupita katika mikoa kuomba kura kwa wananchi na kutoa lugha chafu badala ya kujenga sera itakayoweza kukubalika kwa jamii na kwamba jamii inapaswa kutambua baadhi ya Vyama vya upizanzani havina ofisi za kuendeshea shughuli na kwamba watambue maendeleo hayaletwa kwa kasfa bali kwa sera ya chama husika.
"Kama kweli wananchi mtakuwa na mtazamo viongozi gani wanaoweza kuwaongoza wakiwa ni watu wa kwanza kukashfu nchi na chama je wakiwa madarakani watawaongoza vipi sasa mtambue msimu wa kampeni ndio wanapita kuomba kura wakati wa kampeni hamuwaoni je huu uongozi utatambua kero za wananchi na kuleta maendeleo"Alisema Mwakyusa.
Naye Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, alisema kauli ya Chadema dhidi ya
Mwinyi, wameifananisha na mbio za sakafuni kutokana na dhamila ya ungozi wa chama hicho kumgeukia mwenyewe na kujitukana kutokana na mgombea wake kutolewa katika kinyanganyiro cha ugombea ubunge jimbo la Mbeya vijijini.
Makamba, alisema hakuna haja ya wananchi kukichagua chama cha Chadema na CUF kutokana na kuonyesha nidhamu yao na kwamba hawana uwezo wa kuleta maendeleo kutokana na kuonyesha wazi kashfa ya kumtukana kiongozi wa ngazi za juu ambaye aliwahi kuongoza nchi.
Akizindua kampeni hizo, Mwinyi alisema kuwa Vyama vya Siasa vilipaswa kupanua wigo kwa wananchi kwa kueleza sera za chama husika zitakazokubaliwa na wananchi na kuleta maendeleo .
Alisema vyama vya siasa vinapaswa kushindana katika Sera na si kushindana kwa
matusi, dharau na kejeli.
Alisema kutumia uungwana katika kampeni za uchaguzi vinaweza vikapata fursa ya
uongozi na kutatua matatizo ya wananchi kwa kutumia Sera za Chama husika.
Alisema kuwa vyama vilipaswa kila kinachofanywa kinafanywa kwa kufuata misingi na kanuni za katiba katika kugombea jimbo la Mbeya vijijini ili liwe na Amani Umoja
na Mshikamano na kujenga mzinga wa nyuki ulioshikimana katika kuleta maendeleo
Demokrasi,udugu, na muungano utakaolinda haki za wananchi na kuheshimu ,kuelimisha na kupata misingi bora katika jamii.
"Mimi nimekuja kuzindua kampeni na wala sijaja katika kupiga kampeni na kwamba
niliwashangaa sana viongozi wa chadema kwa kupanga kuja kutukana na matusi na kwamba hakuna chama kinachoendeshwa kwa kukejer na kutoa rugha chafu,"alisema mwinyi.

Saturday, January 3, 2009

CHADEMA Walizwa na NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetupilia mbali rufani ya mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sambwee Shitambala, dhidi ya uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi kumwondoa katika orodha ya wanaowania ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini. Shitambala ambaye aliwasilisha rufani dhidi ya uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Desemba 30, mwaka jana baada ya kuwekewa pingamizi na wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), kwamba alikiuka taratibu za ujazaji fomu hiyo, kwa kuapa kwa kutumia wakili badala ya mahakama kama sheria ya uchaguzi inavyoagiza. Akitolea uamuzi wa rafani hiyo Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Lewis Makame, alisema Tume ilimwita mrufani juzi kwa lengo la kupata maelezo ya ziada kuhusu sababu za rufani aliyowasilisha na kwamba, hayakupishana na yaliyoandikwa. Jaji Makame alisema kwa kuzingatia sababu za rufani, NEC iliona hoja tatu za msingi zilizokuwemo ambazo ni Je, tamko la kisheria lililotolewa na mrufani katika fomu zake za uteuzi ni halali kwa mujibu wa kifungu cha 38(3) (a) cha Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya mwaka 1985? Je, Sheria ya Viapo (The Oath and Statutory Declarations Act (CAP 34 R. E. 2002) na Sheria ya Wanaoidhinisha Viapo (The Notaries Public and Commissiners for Oaths Act (CAP 12 R.E. 2002) zinaweza kutumika katika suala hili? Alisema tatu,Tume iliangalia hoja ambayo wagombea walikuwa na muda wa kutosha wa kukamilisha fomu zao za uteuzi na kuziwasilisha kwa wakati? Aidha, Je,Tume inaweza kutumia ``proviso`` ya kifungu cha 38(4) cha Sheria ya Uchaguzi na. 1 ya mwaka 1985? Alifafanua kuwa baada ya kuzipitia hoja hizo za msingi, NEC ilibaini kuwa mgombea wa Chadema alikiuka taratibu ya kula kiapo kwa wakili aliyemtaja kwa jina la Evarist Martin Mashiba wa S L P 4185 Dar es Salaam na kugongwa muhuri wa wakili huyo na kwamba, kifungu cha 38(3) (a) cha Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya mwaka 1985 kimebainisha tamko linalotakiwa kufanywa na mgombea ubunge. ``Kila fomu ya mgombea uchaguzi lazima iambatane na tamko rasmi la kisheria ambalo limewekwa saini na mgombea mbele ya hakimu likitamka bayana sifa za mgombea na vile vile kutamka wazi kuwa mgombea hana pingamizi kugombea katika uchaguzi,`` alisema. Alisema hivyo katika kifungu hicho neno ``shall`` ndio lililotumika ambalo linaonyesha ni �lazima� mgombea kula kiapo mahakamani na kwa Hakimu Mkazi, Wilaya na Mahakama za Mwanzo hivyo ni dhahiri kwamba, wakili hapaswi kushuhudia tamko husika na tamko hilo litakuwa sio halali. Aliendelea kuwa kipengele cha Sheria za Viapo na Sheria ya Wanaoidhinisha Viapo, hakiwezi kutumika katika suala hilo kwa sababu Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya mwaka 1985 imetamka bayana kuhusu anayetakiwa kushuhudia tamko la kisheria la mgombea. Jaji Makame alisema NEC ilitangaza Desemba 17, wagombea kuchukua fomu na kurudisha Desemba 27, kwa maana hiyo kulikuwa na siku sita za kazi hivyo mahakama zilikuwa zinafanya kazi na wagombea walipaswa kutumia siku hizo kula kiapo kwa hakimu. Pia, Tume hiyo imeridhika na maelezo ya mrufani kuwa hakujiapisha mwenyewe na wala hajaajiriwa na Kampuni ya Evarist Mashiba Advocates kama ilivyodaiwa na mweka pingamizi. Kwa upande wa mgombea wa DP, naye amegonga mwamba rufani yake kama sababu za mgombea wa Chadema. Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Mbunge wa Mpanda Kati, Saidi Arfi, alisema chama kitakaa chini kutafakari uamuzi uliotolewa na Tume kwa sababu, ni pigo kwa demokrasia nchini. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, alisema hivi sasa bado hawajaamua kuunga mkono CUF. ``Kwa kuwa jambo lenyewe limetokea sasa, tutakaa na kisha baadaye kutoa taarifa kamili kwa umma, kwa sasa bado tunatafakari,`` alisema Slaa. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Januari 25, unafuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Vijijini, Richard Nyaulawa (CCM).

Friday, January 2, 2009

Mambo ya Mbeya Vijijini na Uchaguzi wa MP


Date::1/2/2009
Mambo magumu Mbeya Vijijini
*Hatima ya mgombea Chadema leo
Na Brandy Nelson, Mbeya
MAMBO yanazidi kuwa magumu katika mchakato wa uchaguzi mdogo wa mbunge Mbeya Vijijini baada ya kuzidi kwa matukio yanayopandisha joto zaidi la kisiasa mkoani Mbeya na hata maeneo mengine ya nchi.
Kuahirishwa kutangazwa kwa matokeo ya rufaa ya mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sambwee Shitambala, hadi leo asubuhi, kumelimepandisha joto kwenye kinyang'anyiro cha kuziba nafasi iliyoachwa na mbunge wa CCM, Richard Nyaulawa.
Awali ilitaarifiwa kuwa uamuzi wa rufaa ya Shitambala, ambaye alienguliwa kugombea ubunge wa Mbeya Vijijini kwa kuapa kwa wakili badala ya hakimu, ingetolewa jana saa 4:00 asubuhi.
Lakini mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Lewis Makame aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa majibu ya rufaa yatatolewa leo saa 5:00 asubuhi wakati yale ya mgombea wa DP, Ndele Mboma yatatolewa saa 8:00 mchana.
Aliyasema hayo jana majira ya saa 10:00 jioni baada ya wagombea, walioenguliwa na msimamizi wa uchaguzi katika kinayang'anyiro cha ubunge katika Jimbo la Mbeya Vijijini na baadaye kukata rufaa, kuhojiwa na tume yake kwenye hoteli ya Mount Livingstone.
"Tumeshapitia rufaa za wagombea wote na majibu tutayatoa kesho saa 5:00 asubuhi kwa mgombea wa Chadema Sambwee Shitambala na saa 8:00 kwa mgombea wa DP, Ndele Mboma," alisema.
Aidha tume hiyo imeagiza wagombea hao wasiendelee na mikutano ya kampeni za uchaguzi, ikibatilisha uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Juliana Malange, ambaye aliwaruhusu kufanya kampeni wakati wakisubiri majibu ya rufaa zao.
Mgombea wa Chadema alifanya mkutano wa kampeni juzi katika kata ya Utengule, Usongwe.
Akiongea baada ya kutoka kuhojiwa, Shitambala alisema kuwa alipata nafasi ya kutoa maelezo mengi kulingana na kosa lililosababisha aenguliwe katika uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na sheria inavyoelekeza katika masuala ya utoaji wa kiapo.
"Pia wametuhoji kuwa wamesikia kwamba tulifanya mkutano wa kampeni, tukamjibu ndiyo kwa kuwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Mbeya Vijijini alituruhusu kuendelea na kampeni," alisema na kuongeza kuwa maamuzi hayo yalikuwa sahihi.
Shitambala alisema kuwa pamoja na maelezo hayo tume imewataka kutoendelea na kampeni hadi baada ya uamuzi kutangazwa kesho.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinadai kuwa wajumbe wa tume hiyo, walianza mjadala wa rufaa hiyo mara baada ya kuwasili hotelini hapo saa 4:00 na kwamba, kulikuwa na mvutano mkubwa hadi majira ya saa 7:00 usiku wa kuamkia jana.
Inadaiwa kikao hicho kiliendelea tena jana asubuhi hadi saa 9:00 wakati walipowaita wagombea na kuwahoji na kumaliza saa 10:00 jioni.