Monday, December 22, 2008

CCM yampiga chini Makamba-Harakati za Mbeya kupata MP



CCM yampiga chini Makamba
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua mgombea wake wa ubunge jimbo la Mbeya Vijijini na kumwengua katibu wake mkuu, Yusuf Makamba katika safu za mbele za kutetea ushindi katika uchaguzi huo.CCM inafanya mikakati mizito ya kuhakikisha hakianguki kwa mara ya pili mfululizo baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime, ambako CCM iliongozwa na Yusuf Makamba.Kuanguka kwa CCM kulisababisha lawama kubwa dhidi ya Makamba kiasi cha kubashiriwa kuwa mkuu huyo wa zamani wa mkoa wa Dar es salaam angevuliwa ukatibu mkuu wa chama wakati wa mkutano wa Halmashauri Kuu uliofanyika Dodoma karibu mwezi mmoja uliopita.Makamba aliokoka baada ya kikao hicho kuisha bila ya kumjadili, lakini sasa hataongoza kampeni ya kutetea kiti kilichoachwa wazi na Richard Nyaulawa aliyefariki dunia kutokana na kuugua kwa muda mrefu.Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Makamba sasa hatakuwa msimamizi mkuu bali mwangalizi na mwezeshaji wa kampeni."Makamba sasa hatajikita moja kwa moja katika usimamizi wa kampeni hizo kama ilivyokuwa Tarime badala yake atakuwa na kazi ya kuangalia na kuwezesha kampeni hizo," alisema Chiligati.Alisema uamuzi wa kutomuweka Makamba kuwa msimamizi mkuu unatokana na mkakati wa chama hicho kuiachia CCM Mkoa kufanya kazi hiyo, badala ya kuongozwa na CCM Taifa."Makamba atakuwa akienda Mbeya kuwezesha kampeni hizo na kurudi," alisema Chiligati. "Kamati ya uchaguzi ya mkoa wa Mbeya ndiyo yenye jukumu la kusimamia uchaguzi huo."Katika uchaguzi wa jimbo la Tarime, Makamba alilaumiwa kuwa hakufanya jitihada za kuondoa tofauti za makundi yaliyoibuka wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005, moja likidaiwa kuongozwa na Kisyeri Chambiri na jingine likidaiwa kuongozwa na Chrisopher Gachuma.Makamba anadaiwa kuegemea kwenye moja ya makundi hayo na hivyo kuwafanya baadhi ya Wana-CCM kutomuunga mkono mgombea wake, Christopher Kangoye.Makamba pia alidaiwa kutotumia wazawa wa Tarime kwenye kampeni hizo na badala yake kuwatumia wapiga debe waliojiunga na CCM kutoka vyama vya upinzani, huku lawama nyingine zikielekezwa kwa kada huyo kwa kushindwa kwenye uchaguzi licha ya kuwezeshwa kila kitu, zikiwemo helkopta mbili.Kuhusu mgombea wa CCM kwenye jimbo hilo la Mbeya Vijijini, Kapteni Chiligati alimtangaza Mchungaji Luckson Mwanjale kuwa ndiye aliyeshinda katika uteuzi huo uliofanywa na Kamati Kuu ya CCM (CC) jijini Dar es Salaam jana.Alisema Mwanjale amewashinda wenzake kadhaa, akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi mstaafu, Robert Mboma aliyepata kura 164.Wengine walioshiriki katika nafasi ya kugombea kuteuliwa ni Allan Mwaigaga, aliyepata kura 259, Adrea Sayile (229), Diovita Diame (162), Petro Mwashusha (28),Flora Mwalyambi(26), Machael Mponzi (23) na Maria Mwambanga(19).Alisema kampeni za uchaguzi huo wa Mbeya Vijijini zitazinduliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi Januari 4 mwakani.Uchaguzi mdogo jimbo la Mbeya Vijijini utafanyika Januari 25 mwakani kuziba pengo la aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Richard Nyaulawa aliyefariki dunia Novemba mwaka huu kwa ugonjwa wa saratani.Wakati CCM imemteua mgombea wake, Chadema ilimteua Sabwee Shitambala kukiwakilisha katika uchaguzi huo utakaohusisha pia Chama cha Wananchi (CUF). Mgombea wa CUF anateuliwa leo kwenye mkutano mkuu wa CUF wilayani Mbeya Vijijini
window.google_render_ad();

No comments: