Monday, December 29, 2008

Mchakato Wa Uchaguzu Mbeya Vijijini


Chadema Vs CCM in my Home!

http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=8873

Date::12/28/2008
Mgombea wa Chadema awekewa pingamizi
Brandy Nelson, Mbeya
MCHAKATO wa uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Mbeya Vijijini umeingia dosari baada ya mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)Sabwee Shitambala kuwekewa pingamizi na vyama vya CUF na CCM.
Wakati mgombea huyo wa Chadema akiwekewa pingamizi, Chadema imeeleza kumwekea pia pingamizi mgombea wa CCM kwa madai kuwa amesema uongo kuhusu mahala alipozaliwa.
Vuta nikuvute hiyo ilitokea jana katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi huo ambako CUF na CCM wamedai kuwa mgombea wa Chadema ameapa kinyume na taratibu za uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha fomu ya pingamizi hilo mjumbe wa tume ya uchaguzi ya CUF, Hussein Mmasi alisema chama chake kimeamua kumuwekea pingamizi mgombea wa Chadema kutokana na kuapa katika kampuni ya uwakili badala ya mahakama ya wilaya.
"Tumeweka pingamizi kutokana na mgombea wa Chadema kuapa katika kampuni ya uwakili ambako yeye anafanyia kazi. Kufanya hivyo ni sawa na mgombea huyo kujiapisha mwenyewe,"alisema.
Alisema taratibu za kisheria zinawataka wagombea kuapa mahakamani na siyo kwenye makampuni ya uwakili, kwani fomu ya mgombea wa Chadema inaonyesha mhuri wa kampuni ya mawakili ambayo ndiyo anayofanyia kazi.
Madai hayo ndio pia yaliyokifanya Chama Cha Mapindizi kumwekea pingamizi mgombea huyo.
Akizungumza na gazeti hili, Mkurugenzi wa vijana wa Chadema John Mnyika, alikiri kuwepo pingamizi hilo na kueleza kuwa chama kimejipanga kulipangua.
Alisema viapo vilikuwa wazi na Chadema imejipanga kuliondoa pingamizi hilo.
Akizungumzia suala la pingamizi la mgombea wake, Mnyika alisema limewekwa kimakosa kwani mawakili ambao ni makamishna wa uchaguzi wa wilaya wanaruhusiwa pia kuwaapisha wagombea.
Alisema mgombea wa Chadema alilazimika kuapishwa na wakili kutokana na mahakama kufungwa siku za sikukuu.
Katika hatua nyingine Chadema kimemwekea pingamizi mgombea wa CCM Mchungaji Luckson Mwanjali kwa madai kuwa mgombea huyo alitoa taarifa za uongo kuhusu mahali alipozaliwa.
Akizungumzia pingamizi hilo mjumbe wa kamati kuu ya Chadema na ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mpanda Kati, Said Arfi alisema wameamua kutoa pingamizi hilo kutokana na mgombea huyo kutoa taarifa ya uongo kuwa ni mzaliwa wa Igawilo kitongoji cha Uyole jijini Mbeya huku taarifa zinaonyesha kuwa ni mzaliwa wa Tukuyu wilayani Rungwe.
"Tumeamua kuweka pingamizi dhidi ya mgombea wa CCM kutokana na kuwepo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa sababu za uongo za mahali alipozaliwa na tumemtaka mgombea huyo awasilishe vielelezo vitakavyothibitisha sehemu halali aliyozaliwa,"alisema.
Alizitaja sababu nyingine za pingamizi hilo kuwa ni Mgombea huyo kutotoa tamko
la kisheria kuhusu maslahi yake katika hospitali teule ya Wilaya ya Mbeya ya Ifisi
na kwamba siye mgombea aliyethibitishwa na chama chake cha CCM.

No comments: