Friday, December 12, 2008

Mbeya Rural Constituency(My Home) Struggling to get New MP!
After The Death of the former MP in my place now people struggle to get new MP to cover the gap,Hope that this can be some efforts towards changing the life of the suffering Mbeya Rural
District residents!But this might be hard as the most of the people in the don't open their eyes
to see who can help them and also some even don't know that they got problems!
The kids in the picture above deserve a bright future,all this lies on the people who have the
dhamana including the MP's.It pains me a lot when i see at the end of the day all these kids
end up nowhere,They even don't how the other kids on the other world live.But one day I
believe more of those will have better opportunities!God help them!
Afisa Elimu wa Chunya achukua fomu kuwania jimbo la Nyaulawa 2008-12-12 13:01:23 Na Thobias Mwanakatwe, Mbeya
Afisa Elimu wa Wilaya ya Chunya mkoani hapa, Petro Mwashusa amekuwa mwanachama wa sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuchukua fomu za kuwania ubunge katika jimbo la Mbeya Vijijini. Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya Vijijini, Hassan Dumwali, alisema Afisa Elimu huyo ambaye ni mkazi wa Mbeya Vijijini, ni mwanachama pekee aliyechukua fomu jana kwani hadi kufikia saa 10:00 jioni ambao ndio muda wa mwisho kwa wanachama kuchukua fomu. Wanachama wengine waliokwishachukua fomu ni Djovita Diame ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mchungaji Langson Mwanjali (Katibu wa Fedha na Uchumi), Aran Mwaigaa (Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa). Wengine ni Flora Mwaliambi (Mjumbe wa Halmashauri (CCM Mbeya Vijijini) na Michael Mponzi ambaye ni mtoza ushuru kituo cha Igoma katika Halmashauri ya Mbeya Vijijini. Wakati wanachama wa CCM wakiendelea kuchukua fomu, kwa upande wa Chadema ndiyo kinaanza leo kutoa fomu kwa wanachama wake wanaotaka kuwania ubunge. Katika kuupa nguvu uchaguzi huo, tayari viongozi wandamizi wa Chadema toka makao makuu wameshawasili mjini Mbeya kupanga mikakati ya jinsi chama chao kitakavyoshiriki uchaguzi huo na kuibuka na ushindi. Viongozi hao bado hawajaanza mikutano ya hadhara na badala yake wanachokifanya kwa sasa ni kuitisha vikao vya ndani vya chama. Kwa upande wa Chama cha Wananchi (CUF) kimeanza kutoa fomu kwa wanachama wake wanaotaka kugombea ubunge ambapo hadi sasa Mwenyekiti wa Mbeya Vijijini wa chama hicho, Amina Ahmed ndiye mwanachama pekee aliyechukua fomu. Naye Kamishina wa NCCR Mageuzi, Adam Mwansampeta alisema chama chake kinaendelea na mikakati kwa ajili ya uchaguzi huo ingawa bado hakija weka wazi kama kitasimamisha mgombea wa ubunge wa jimbo hilo.

No comments: