Tuesday, January 6, 2009

Mboma: Kitambi kimeniangusha

mambo ya Home!
Mboma: Kitambi kimeniangusha
Hawa Mathias, Mbeya
ALIYEKUWA Mkuu wa Majeshi Nchini, Meja Jenerali, Robert Mboma, amesema anaamini kitambi alicho nacho kimesababisha kushindwa katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) za ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini.
Mboma aliyasema hayo juzi wakati akiwashukuru wananchi katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho za kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo.
Alisisitiza kuwa anaamini kilichochangia kutopata kura nyingi zaidi ni kitambi
hicho alichokuwa nacho na kwamba hali hiyo itamkomaza kisiasa.
Mboma ambaye aliwashangaza baadhi ya watu walioshuhudia uzinduzi wa kampeni hizo uliofanywa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi katika kijiji cha Ilembo Mbeya vijijini.
alisema kkuanguka kwake katika jimbo hilo kumetokana
na wananchama wa chama hicho kumnyima kura.
Alisema kitendo hicho hakiotamuathiri bali wanamkomaza kisiasa na kwamba endapo kama angeteuliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo angelepeleka maendeleo.
"Kwa kweli nanawashukuru wananchi mlionipigia kura nilizozipata ingawa hazikuwa
ndogo lakini ninasikitika na ninawashukuru ambao hawakunipigia kura na kuniangusha wakati wakijua wazi kuwa mimi ni mzaliwa na hapa na mngenichagua ningewaletea wananchi maendeleo katika jimbo la Mbeya vijijini," alisema.
Aliendelea kusema kuwa sio mbaya hata kama wamemchagua Mchungaji Mwanjali kwa sababu anaimani atawaletea Maendeleo na kurithi yale yote aliyatarajia
kuyafanya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Marehemu Richard Nyaulawa katika
kuboresha huduma za jamii hususan maji, umeme na kuboreshea miundombinu.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya David Mwakyusa aliwatahadhalisha wapiga kura kuwa makini na Vyama vya Siasa hususan Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) a kwa kuzingatia sera zao na kwamba wawafananishe na Vyura wanaosubili kipindi cha Mvua na kuanza kukoroma katika mito.
Alisema vyama vya upinzani vinatakiwa kuangaliwa kwa umakini na kwamba kipindi hiki cha kampeni wanaanza kupita katika mikoa kuomba kura kwa wananchi na kutoa lugha chafu badala ya kujenga sera itakayoweza kukubalika kwa jamii na kwamba jamii inapaswa kutambua baadhi ya Vyama vya upizanzani havina ofisi za kuendeshea shughuli na kwamba watambue maendeleo hayaletwa kwa kasfa bali kwa sera ya chama husika.
"Kama kweli wananchi mtakuwa na mtazamo viongozi gani wanaoweza kuwaongoza wakiwa ni watu wa kwanza kukashfu nchi na chama je wakiwa madarakani watawaongoza vipi sasa mtambue msimu wa kampeni ndio wanapita kuomba kura wakati wa kampeni hamuwaoni je huu uongozi utatambua kero za wananchi na kuleta maendeleo"Alisema Mwakyusa.
Naye Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, alisema kauli ya Chadema dhidi ya
Mwinyi, wameifananisha na mbio za sakafuni kutokana na dhamila ya ungozi wa chama hicho kumgeukia mwenyewe na kujitukana kutokana na mgombea wake kutolewa katika kinyanganyiro cha ugombea ubunge jimbo la Mbeya vijijini.
Makamba, alisema hakuna haja ya wananchi kukichagua chama cha Chadema na CUF kutokana na kuonyesha nidhamu yao na kwamba hawana uwezo wa kuleta maendeleo kutokana na kuonyesha wazi kashfa ya kumtukana kiongozi wa ngazi za juu ambaye aliwahi kuongoza nchi.
Akizindua kampeni hizo, Mwinyi alisema kuwa Vyama vya Siasa vilipaswa kupanua wigo kwa wananchi kwa kueleza sera za chama husika zitakazokubaliwa na wananchi na kuleta maendeleo .
Alisema vyama vya siasa vinapaswa kushindana katika Sera na si kushindana kwa
matusi, dharau na kejeli.
Alisema kutumia uungwana katika kampeni za uchaguzi vinaweza vikapata fursa ya
uongozi na kutatua matatizo ya wananchi kwa kutumia Sera za Chama husika.
Alisema kuwa vyama vilipaswa kila kinachofanywa kinafanywa kwa kufuata misingi na kanuni za katiba katika kugombea jimbo la Mbeya vijijini ili liwe na Amani Umoja
na Mshikamano na kujenga mzinga wa nyuki ulioshikimana katika kuleta maendeleo
Demokrasi,udugu, na muungano utakaolinda haki za wananchi na kuheshimu ,kuelimisha na kupata misingi bora katika jamii.
"Mimi nimekuja kuzindua kampeni na wala sijaja katika kupiga kampeni na kwamba
niliwashangaa sana viongozi wa chadema kwa kupanga kuja kutukana na matusi na kwamba hakuna chama kinachoendeshwa kwa kukejer na kutoa rugha chafu,"alisema mwinyi.

No comments: